Katika sura tofauti.wanaunganishwa na SURA YA MUNGU. |
……………leo tunafikia tamati ya somo
letu,katika majuma mawili yaliyopita tumeona kwa undani nini maana ya “Sura ya
Mungu” na maelezo ya kutosha kuhusu faida na namna sura ya Mungu inavyotenda
kazi kazi kwa wanadamu.Katika kuhitimisha tutaanza na mtazamo wa mwisho kabisa
baada ya UTAKATIFU(wiki ya kwanza),KIBALI (wiki ya pili).
MAMLAKA.
Neno hili linaweza kutafsiriwa
kama,nguvu,uwezo,madaraka ya kufanya jambo fulani.Katika maana ya kiingereza
linaweza kutamkwa (authority, jurisdiction,
mandate).Ni dhahiri kuwa mtu yeyote aliyepewa mamlaka atakuwa na nguvu ya
kufanya jambo lolote lililo katika uwezo wake tofauti na mtu asiye na
mamlaka.:divyo ilivyo kwa mtu aliye na sura ya baba yake ana mamlaka kubwa kwa mali alizo nazo baba
yake na kila kitu kinachomhusu baba yake.Hebu tutazame maamuzi ya wafanyakazi
(wakulima) hawa katika Mathayo 22:38-39,walimmuua motto wa mwenye shamba kwa kuwa walijua ana mamlaka juu ya shamba
lile.Na katika upande wa MUNGU ni vivyo ivyo wale wenye sura ya MUNGU wanakuwa na mamlaka ya kufanya vitu vingi na
vikubwa zaidi.N a tuanze kumwangalia YESU
akitabiriwa kupewa mamlaka na baba yake,(Isaya 9: 6-7)..Katika mistari
hiyo tunaona YESU akitajwa kama mshauri
wa ajabu,Mungu mwenye nguvu,baba wa milele,mfalme wa amani,hakimu n.kHii yote
inatokana na kuwa na sura ya baba yake.(Rejea
SEHEMU YA KWANZA YOHANA 5:19 “as
Son as Father”)..Mathayo 9:1-6, makutano waliulizana maswali juu ya kitendo
cha YESU
kumsamehe mtu dhambi,ila jibu lake lilikuwa wazi kuwa mwana anayo amri
(authority) kusamehe.Mathayo 8:27 inaonyesha mshangao walioupata wanafunzi wa
YESU,baada ya YESU kutuliza dhoruba
“Huyu ni mtu wa namna gani hata
pepo na bahari zimtii?”.Ni mamlaka aliyo nayo mwana yanamfanya aweze kutuliza
dhoruba.
HITIMISHO:
“it is the process” unaweza ukakuta mtu
sura yake inabadilika kila iitwapo leo,labda kwa kuwa amepauka au mafuta
anayotumia hivyo kupoteza sura yake ya asili au ambayo kafanana na baba
yake.Hivyo ndivyo ilivyo kwa maisha yetu ya kiroho,tunahitaji kutunza
wokovu,utakatifu ili sura zetu ziwe zile za asili…” Heri wazifuao nguo zao,
wawe na amri kuundea mti wa uzima,kuingia mji wa malango yake” Ufunuo 22 :14
###baraka ziwe kwako rafiki,kwa
kufuatilia somo hili kwa ukaribu zaidi”
Kaizer Xavier Msosa
0716047700.0759302486
No comments:
Post a Comment