Lizick mwashambwa ..(aliye kushoto)
NDOA NA UCHUMBA
Math
7:21- yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu ndiye atakaye okoka.
Luka
6:46(kufanya maagizo ya Mungu)
Moja
ya mapenzi ya Mungu ni kuona watu wanaoa na kuolewa, hivyo kuhitaji kuoa au
kuolewa si dhambi madam zingatia (Mhu 3:1). Hata hivyo biblia haijaweka wazi
kwamba ni kwa wakati gani au umri gani inatakiwa mtu aoe au kuolewa ila cha
msingi ni kutambua kwamba Mungu ni wa utaratibu(1Thes 3:6-7). Hata hivyo,
haitoshi neon la Mungu linasema ‘’KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA’’(Mith
1:7), nini maana ya neon ‘maarifa’, zipo maana nyingi za neon maarifa, miongoni
mwazo ni; akili ya ugunduzi, hivyo wewe mwenyewe kama mtu uliye okoka na mwenye
maarifa unapaswa kugundua wakati wako wa kuoa au kuolewa kwa kuwa ni miongoni
mwa kutimiza mapenzi ya Mungu, hivyo kutohitaji kuoa au kuolewa wakati una sifa
za kufanya hivyo ni kudharau mapenzi ya Mungu wazi wazi na kibaya zaidi
unajikuta unaangukia katika uasi wa macho na mawazo(Math 5:28). ZINGATIA: hata
hivyo watumishi wa Mungu husema kuhitaji kuoa au kuolewa ni WITO. Hata mimi kwa
ufahamu wangu nakubali hiyo dhana kwani unakuta mtu ni Yule Yule siku zingine
zote alikuwa hahitaji suala hilli mbali na hapo alikuwa hataki kuzungumzia
na kusikia habari yoyote kuhusu jambo
hili. Lakini wio wake ukifika utamuona yeye mwenyewe anaanza kuhitaji
,kuzungumzia na hata kupenda kusikia habari hizi, hivyo kwa mtu huyo ajue
tayari kwa wakati umefika akiachana na vipindi vya mpito vya ukuaji wa mwili
kwa maana ya balehe na kupevuka kwa kuwa hiki ni kipindi hatari sana ambacho
kijana mara nyingi huendeshwa na mawazo ya kawaida na hisia za mwili kabisa(Gal
5:19).
LAKINI,
nasikitika kwa vijana wenzangu ambao wamejitunza katika maisha ya kiroho na
kimwili tangu walipookolewa, lakini wakifikia kipindi hiki cha kupata wito wa
kuoa au kuolewa huwa wanajiuliza yafuatayo;
a) Tumevamiwa
na shetani
b) Tumeanza
kurudi nyuma
c) Tunaelekea
kutenda dhambi
d) Tumeanza
kupenda dunia
Hata
hivyo wengi wetu huanza kuikataa hali hiyo na kuikemea kwa gharama kubwa hata
kwa kufunga na kuomba. Lakini kwa kuwa neon la Mungu linasema ‘’kwa kuwa
umekataa maarifa name nimekukataa wewe’’(Hosea 4:6-8), nasikitika kusema
kwamba, kwa kuwa hapa yunapingana na mpango wa Mungu, mwisho wa vijana wengi
waliookoka na si kuokoka tu na hata walioonja neema ya kuitwa watumishi wa
Mungu huwa wanarudi nyuma kwa kasi kubwa na kuacha jamii, kanisa, wazazi na
marafiki wetu wameshika tama zao na vidonda visivyo ponyeka mioyoni mwao na
kukamilisha msemo usemwao na wengi wanaodhihaki wokovu kwamba huwezi kuokoka ukiwa kijana au kuokoka ni hatua ya kupitia katika maisha ya
mwanadamu kama ilivyo kutambaa kwa motto mdogo n.k
Lakini
kukataa wito huu wakati unajua ni agizo la Mungu(Mwa 1:29) ni sawa unahisi njaa
baadala ya kuomba msaada wa chakula unaanza kukemea sijui kama unaweza
kufanikiwa.
Samahani
kwa wachungaji na watumishi wa Mungu wengine kwa kuwa nami ni kijana sikupaswa
kuandaa somo hili, lakini kulingana na jambo hili linavyo athiri vijana
wenzangu kwa kasi ni kubwa mpaka sasa kuna vijana wenzangu wengi waliorudi
nyuma, lakini zaidi wako vijana watatu wameshapotea kabisa katika huduma.ila
ungepata neema ya kuyajua maisha yao kabla ya kurudi nyuma ungelia machozi na
siwezi kuwasahau kwa jinsi ambavyo tulishirikiana nao katika kumtumikia Mungu.
Ni kwa sababu ya usalama tu majina yao yamehifadhiwa ningewataja dhahiri.
Hivyo, nimepata msukumo wa kuaandaa somo hili sijui kama ni mawazo yangu au ni
maelezo ya Mungu. lakini katika yote mungu anihurumie na kuniongezea neema.
Ndugu
zangu vijana mliookolewa ikumbukwe kwamba pamoja na kuokoka mwili huwa unabaki na utaratibu wake wa kawaida. Kinacho
takiwa ni kuushinda, katika somo la baiolojia tunasema kinacho takiwa ni
kuufanya mwili kuwa recessive na
roho kuwa dominant, hata hivyo kuna baadhi ya kanuni za mwili huwa
zinabaki pale pale kama kuhitaji kula, kuoga , kunywa, kulala, kuvaa n.k. cha
msingi kupitia (Mith 1:7) unapaswa kujiuliza yafuatayo kulingana na mifano
tajwa hapo juu
I.
Unatakiwa kula nini na kwa mda gani?
II.
Unatakiwa kuoga nini na wapi?
III.
Unatakiwa kunywa nini na eneo gani?
IV.
Unatakiwa kulala wapi na mda gani?
V.
Unatakiwa kuvaa nini, wapi na kwa mda
gani(Math 6:15-19)
Kadhalika
mwili huwa unafika mahali unahitajikukamilishwa kwa kuoa au kuolewa(Mwa
2:21-24). Cha msingi hapa ni kwamba kuhitaji kupata mwenzi wa maisha si dhambi
ila nani wa kuwa mwenzi wako, yuko wapi, utampataje na ni lini? Katika maswali
hayo na mengine mengi ambayo vijana huwa tunajiuliza katika eneo hili basi karibu
tufuatane hapa chini na tuone namna ya kupata majibu.
A. IMANI
NA SUBIRA KATIKA KUOA NA KUOLEWA
Baada
ya kuona kwamba kuhitaji kuoa au kuolewa
siyo dhambi bali ni hatua ya kupata mwenzi wako katika maisha(1Kor 11:11). Cha
msingi unapaswa kuwa na subira pamoja na imani(Ebr 11:1-6) ZINGATIA , vyovyote vile tulivyo lazima tuamini kwamba
kila kaka ana mke wake na kila dada ana mme wake mmoja katika Bwana na yupo
mahali flani hata kama bado hatuja wafahamu katika macho ya kawaida na bila
kujali falsafa ya takwimu za dunia kwamba wanawake ni wengi kuliko wanaume. HAPA
MWAMINI MUNGU KUWA YUPO MWENZI WAKO HATA KAMA HUJUI ALIKO AU NI NANI
a) Bila
kujali gharama za maisha au uchumi wako
b) Bila
kujali sura, umbile, rangi, kimo, kabila, asili, elimu,au ulemavu wako yupo wa
kufanana na wewe(Mwa 2:18) NB: mimi binafsi najua Mungu humtoa mtu chini na
kumpeleka juu, wengine wanakataa kuolewa au kuoa kwa kuangalia vigezo vya
uchumi, gari, elimu nk. Lakini shuhuda za wengi waliofanya jambo hili katika
njia za Bwana wanasema maisha mazuri ya ndoa ni yale watu wanaanza chini na
kwenda juu.
B. IMANI
YA MUNGU NI LAZIMA IAMBATANE NA SUBIRA
pamoja na uzuri wa jambo hili la kuoa au kuolewa katika Bwana ni lazima
kabla ya tendo hilo mhusika awe binti au kijana asubiri kwanza wakati Mungu
anafanya mpango kwa ajili yake(Yak 5:11)
HAPA NDIPO VIJANA WENGI TUNAPO KOSEA,
njia pekee ya kupata mwenzi wako wa maisha ni KUOMBA KWA IMANI TU, hata
hivyo kwa binti akiomba hata akipata msukumo juu ya kijana flani haruhusiwi
kwenda kumwambia ila asubiri, kwa upande wa kijana wa kiume zipo hatua tatu za
kufuata (1)kuomba (2)kutafuta kwa maelezo
ya Roho mtakatifu (3) kutoa taarifa kwa binti, baada ya kutoa taarifa kwa
binti, binti mwenye busara na makini hata kama anajua ndiye aliye pata msukumo
kwake ataomba mda wa kwenda kumuuliza Mungu kwa usahihi zaidi, ila siyo kuleta
usumbufu usiokuwa na maana na wewe kaka ukisha ambiwa subiri siyo kukasirika na
kuchukua maamuzi ya haraka. Binti baada ya kumuomba Mungu kwa usahihi na
kujua kwamba jambo hilo ni kweli unapaswa kutoa taarifa kwa UTARATIBU. Ni
vizuri taarifa zipitie kwa watumishi wa Mungu kwanza ili wawape utaratibu namna
ya kwenda na jambo hili kabla ya ndoa maana
uzoefu unaonyesha kwamba baada ya hawa wawili kuridhiana huwa kunakuwa
na raha ya ajabu ambayo inaweza kuwapelekea katika kumkosa Mungu wakikosa
usimamizi wa karibu wa watumishi wa Mungu wakati wa uchumba wao(Math 7:7).
USHAURI-kwa
kuwa jambo hili utafiti wa kisasa unaonyesha kwamba watu wengi wakiwemo wenye uchumi wa juu na walio
na elimu ya juu walishashindwa kabisa na kujikuta wanalia kilio kisicho na
msaada “MAJUTO NI MJUKUU” hivyo mshirikishe baba yako wa kiroho pamoja na
watumishi wa kweli wa Mungu wachache ili usije ukakwea penginepo(1Sam 3:1-11).
Samahani
sitazungumzia kwa undani juu ya ndoa ila niombee siku nikipata neema
nitazungumzia hilo, lakini kwa kifupi kwa kuwa uchumba unatupelekea kwenye ndoa
ni muhimu ujue misingi mikuu mitano ya ndoa ya mtu aliyeokoka.
I.
Wote wawili wawe hawajawahi kuingia
katika ndoa, au mmoja wapo au wote wamefiwa na wenzi wao na si VINGINENYO.(1kor
7:8-9,38-39)
II.
Ruhusa ya binti (Mwa 24:57-58)
III.
Ruhusa ya wazazi wa binti- inaweza
kuambatana na kutoa mahali maadam uruhusiwe na wazazi wa binti, hata usipo toa
mahali lakini ukiruhusiwa na wazazi wake haina shida, hakuna kipimop maalum cha
mahali itategemeana na utakavyo jieleza (1Kor 7:36)
IV.
Baraka za wazazi wa rohoni(Mwa 1:27-28,
Hes 6:24-27)- huu msingi wa nne ni kwa watu waliookoka na ni muhimu sana kuliko
unavyo dhani. Baada ya watu kufunga ndoa wakiwa kanisani au mahali pengine ni
MWIKO kusema nilikosea kwa hiyo nafunga ndoa tena huo ni UZINIFU zaidi ya ule
unaofanywa na mataifa,
V.
Kuambatana katika maisha kwa maana ya
kuwa mwili mmoja(Mwa 2:24) TAHADHARI- MWIKO MWEBRANIA KUWA KATIKA MAHUSIANO YA
KIMAPENZI(UCHUMBA) NA MMISRI, MWISRAELI NA MYEBUSI(2Kor 6:14-18); katika
tahadhari hii ukumbuke kilicho mtokea SAMSONI kwa DELILA na kilicho mtokea
SULEMAN kwa wanawake wa kigeni(wasiookoka)(1Fal 11:1-4, Amu 16:1-31)
Nimalizie
kwa kukutia moyo binti au kaka kama utapata mwenzi wako ambaye ni mcha Mungu
yaani anaye mhofu Mungu kuna faida kubwa sana za kiroho na kimwili neon la
Mungu linasema hayo na watu wachache wal;iofanikiwa katika hili suala, hizi ni
baadhi ya faida hizo
a) Nguvu
za kiroho huongezeka pale tunapokuwa wawili yaani mme na mke katika Bwana kwa
kupitia faraja, ushauri na ushirikiano na kinyume chake linaweza kuwa jibu(Kumb
32:30, Yosh 23:10, Mhu 4:9-12)
b) Utapata
nguvu zaidi ya kushinda dhambi inayotesa ulimwengu kipekee, zinaa au
uasherati(1Kor 7:1-7).
MWISHO-
UBARIKIWE KIJANA MWENZANGU, Mungu akinipa
neema tutaonana kwa miaka ijayo katika somo liitwalo “MALIPIZO YA NDOA”
Ni mimi
Mtumwa wa Yesu………….
Mwashambwa N
Liziki
Kwa
maswali, maoni na msaada wa maombi tumia
0752 267 292, P.O.BOX 85 MBEYA, lizikineckson@gmail.com
No comments:
Post a Comment