SEHEMU YA PILI (2).
Wiki
iliyopita tuliachia katika maana ya Agano,Wiki hii tunaendelea kuona jinsi
maagano ya kibinadamu yanavyowekwa pamoja na maagano ya ki MUNGU yanavyowekwa.
A: MAAGANO YA KIBINADAMU
Maagano
ya kibinadamu ni makubaliano yanayofikiwa baina ya watu kila upande upande
ukiwajibika kutimiza makubaliano yaliyopo katika Agano lao.
Maagano yanawekwa
katika mazingira gani?
Maagano
yanawekwa katika hali ya utulivu pasipo
kulazimishwa.Lugha ya kisheria inaonyesha mkataba uwekwe pasipo (Fraud,Misrepresentation,Undue
influence.)
Kitu gani
kinalinda Agano (Makubaliano)?
Makubaliano
yanalindwa na aidha katika karatasi (document) maalumu ambayo kila upande
unabaki na nakala (copy) moja..Mahakama itaangalia nakala za makubaliano yale,ili
kumtia hatiani Yule aliyeshindwa kutimiza yale yaliyo katika makubaliano.
B:MAAGANO YA KIMUNGU
Ni patano
kati ya mtu na MUNGU.Kwa watu wengi haieleweki,wengi wanajiuliza ni jinsi gani
MUNGU anaweza kuweka agano na mwanadamu.Ila ni ukweli kuwa walioweka maagano na
MUNGU walipata faida kuu,angalia (
Nehemia 1:2-11,7:1-3)
Maagano
yanawekwa katika mazingira gani?
Maagano
ya ki MUNGU yanawekwa katika MAOMBI,maana ndipo tunapoweza kusema na MUNGU
wetu.Kama ilivyo katika makubaliano ya kibinadamu hata katika maombi pia
utulivu unahitajika maana yale mtakayokubaliana ndiyo yatakayopaswa kufuatwa.(Mwanzo 24:43-48).
Kitu gani kinalinda Agano
(Makubaliano)
Maagano
ya ki MUNGU yanalindwa na kutunza yale uliyomuomba MUNGU.Tazama Isaya 43:26 “unikumbushe” ina maana utunze agano “maombi”.
Itaendelea……….
Uchambuzi mzuri sana huu ubarikiwe!
ReplyDelete