Thursday, January 18, 2018

INUKA, SIMAMA, SONGAMBELE

Umewahi kujilaumu pale ulipokesea? Maamuzi yaliyokupelekea kuwa hivyo ulivyo, na mengine mengi.Wengi wetu tunatumia muda mwingi sana kujilaumu na kulaumu wengine kuwa ni chanzo cha sisi kutosogea mahali na eneo tunalotamani tuwe.Ukianguka mahali leo hii chukua hatua ya kujiuliza nn kilikufanya uanguke, inuka, simama, jipange.Bwana bado ni mwema kwetu.


Thursday, December 24, 2015

HERI YA CHRISTMASS NA MWAKA MPYA

Hello ambassadors of christ! Bwana YESU asifiwe sana...!!, Nafurahi sana kutambua kuwa bado mnamuinua kristo ambaye ndiye wokovu wetu., kwa ufupi sana natambua kuwa yeye alikuja ulimwenguni..
1. Ili asiwepo wakupotea hata mmoja, Bali wote tuifikie toba ya kweli. yohana 3:16, Ebrania 3:35-36, warumi 10:9
2. Ili tuishi maisha ya ushindi, amani (isaya 9:6) na pia yaweze kubadilika zaidi, mathayo 11:28
3. Ili tuponywe magonjwa yooote, mathayo 9:2...., zab 103:3


therefore, ni muhimu kusimama imana, kuukomboa wakati nakumtangaza kristo zaidi na zaid, sio magamba tu, au tukaishia malibwi na mgwashi NOOOO.. Bali tutanue mipaka na vision zaidi hata sehemu zisizofikika ili nao wamjue kriso aliye HAI.

Thank you vry much,, nawatakia christmass njema na yenye baraka,na sio X-MASS.Mic you all
posted by
pst. festo.0716916244

Tuesday, September 8, 2015

MAHUSIANO YALIYOPO KATI YA MAOMBI NA KUSAMEHE

Hello christ ambassadors, nawasalimu katika jina la YESU kristo aliye hai. nafurahi kukutana nanyi kupitia blog hii muda huu, MUNGU akubarki sana kwa kuamua kusoma post hii, bila kusahau shukrani zangu za dhati kwa viongozi wa casfeta SEKOMU kwa ujumla wao.Naamini kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU aliyenisukuma kuandaa somo hili utapokea kitu kikubwa sana juu ya maombi na kusamee, Twende pamoja...

KUSAMEHE kwa namna rahisi sana yakueleweka naweza kusema ni;
KUACHILIA, KUSAHAU AU KUTOKUKUMBUKA KITU AMBACHO ULIFANYIWA VIBAYA AU MTU ALIKUKOSEA.Yamkini kilisababisha maumivu sana moyoni mwako,ulilia sana, ulijiuliza sana,why this happen... why, lakini ile hali yakuyashinda hayo maumivu na hizo aibu nakukubali kuachilia na kusahau kabisha hapo tunasema UMESAMEHE.Na ndo mana KUSAMEHE means FORGIVENESS hii inadefiniwa kama "STOP filling angry toward someone"

Now; kuna mahusiano makubwa sana (relationship) kati ya MAOMBI NA KUSAMEHE.
"MARKO 11: 25-26.... Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]"

"MATHAYO 6:9-12....9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.11 Utupe leo riziki yetu.12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

Nii tunajifunza hapa;
1. kuna maombi mengine tunaomba sana lakin tunashindwa kupokea ONLY kwa sababu , hatuna roho ya kusamehe ndani yetu.
2. vile ambavyo tunasamehe watu wengine ndivyo MUNGU pia anatusamehe makosa yetu


Ukisamehe(ukaachilia na kusahau)lile ulilotendewa, wewe pia unayo nafasi kubwa sana yakusamehewa sawa sawa na neno la MUNGU.
Usiposamehe(nimekusamehe lakini sito kusahau..)tambua kuwa nawewe huna msamaha mbele za BWANA.

"WAEBRANIA 12:14 ...Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote...." Kujibiwa maombi yetu kunategemea sana mahusiano (amani, maelewano) tuliyonayo na watu wengine, Ila kumbuka pia 1 yohana 3:4.... "Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi" sasa basi tusipo samehe- tunabaki na uasi, uasi ni dhambi na dhambi inatutenga na uso wa MUNGU "ISAYA 1:15-17"

Swali dogo kwetu;

....kama MUNGU ameagiza kabla ya kuomba lolote ni lazima tusamehe kwanza/tusiwe na neno na mtu yeyote Je, inakuwaje tunataka kujibiwa haja zetu za masomo(kupandisha GPA,Kutopata sup, carry)kupata mke/mmekazi n.k kabla yakusamehe wengine kwanza?????? kumbuka ndugu yangu mpendwa point za pale juu lakini pia maombi yetu mengine hayajibiwi kwa sababu TUMEWAJAZA WATU MIOYONI MWETU KWA KUTO KUSAMEHE....

Mda wangu ni mchache na upo fixed sana sana, hata kufikia hpa namshukuru MUNGU,Labda kabla yakuhitimisha tuone nini cha kufanya kwa ufupi tu.
1. fanya toba ya kweli kama ROHO wa MUNGU anakushuhudia kuwa eneo hili la kusamehe ni shida kwako,
2. Anza kumwomba MUNGU kwa juhudi ili roho ya kusamehe nakuachilia ijengeke ndani yako
3.Usitenganishe kusamehe na kusahau

.....BARKIWA SANA MTU WA MUNGU,Nakupenda sana.. kwa leo naomba niishie hapa
Prepared by Pst.SHIJA, festo.
email; festojs@gmail.com