mzawa wa injili
MAHUSIANO
Mzawa wa injili,,
ninawakaribisha katika kulianza somo letu zuri la mahusiano. Kwa undani zaidi
kuhusu somo hili na mengine mengi kuhusu mzawa wa injili tembelea live bila chenga gospel
blogspot.com au mzawa wa injili gospel forever blogspot.com.
UTANGULIZI
Mahusiano ni muhimu
na lazima katika maisha. Hatuwezi kuishi pasipo mahusiano. Hata hivyo,
mahusiano yaweza kuwa dhana ya kutuumiza au kutupa amani na hii hutegemeana na aina ya mahusiano husika.
Katika somo hili Mungu amenipa Neema kuzungumzia kwa undani mahusiano juu ya vijana ambao hawajaoa ama
kuolewa… unajua ni kwa nini (1Yoh 2:14),, vijana wanazo nguvu na hivyo Mungu
anahitaji awatumie, lakini shetani anahitaji awatumie pia. Na pia biblia
inatuonya kumkumbuka Mungu siku za ujana wetu (Mhu 12:1).
Mahusiano
mabaya na mazuri
Ni swali ambalo
liko katika vichwa vya watu wengi,, yapi ni mahusiano mazuri au mabaya kwa
kijana. Ndugu zangu, katika mtazamo wa Biblia nitaeleza kidogo na ROHO akupe
neema ya kuelewa. Vijana wengi waliookoka wamejikuta wakianguka katika dhambi
kwa kushindwa kuchagua kwa usahihi ni aina gani ya mahusiano wawe nayo.
Vifuatavyo ni baadhi ya vigezo unavyoweza kutumia kujua kama mahusiano uliyo
nayo ni sahihi au siyo.
Yanampendeza
Mungu?
Kila jambo linalo
fanyika nje ya upendo wa Mungu ni dhahiri kuwa litampelekea mhusika katika
majuto na aibu. Unaweza kulipima hili kupitia usemi na mwenendo wenu kwa ujumla
katika mahusiano yenu. Biblia inasema mazungumzo mabaya huharibu tabia
njema(1Kor 15:33). Mazungumzo mabaya,na dalili yoyote ya dhambi itakupelekea
kumkosea Mungu na kujutia maamuzi yako. Kwa hiyo, mahusiano yoyote ambayo yako
nje ya kusudi la Mungu hayafai na yanapswa kuepukwa. Tumia muda mwingi katika
kuomba na Mungu lazima akuonyeshe cha kufanya.
Una amani
ya kristo?
(Kol 3:15)..Ni
lazima pia upime kama amani ya kristo ina ruhusu wewe kuwa katika mahusiano
hayo. Hapa pia naomba nieleweke kuwa si kila amani iliyo ndani yako yatoka kwa
kristo. Kuna watu wanaotumia mwanya huu kujihalalishia mahusiano yasiyo halali
kwa kudai kuwa amani ya kristo ina waruhusu kumbe ni matakwa yao na mwisho wao
huwa ni kujuta tu. Naomba nikupe ushuhuda huu “ nikiwa kidato ch nne, binti
mmoja alinifuata na kuniomba ushauri juu ya kijana mmoja aliye kuwa anamfuata akitaka
kumuoa ila alikuwa hajaokoka. Binti Yule nilipomuuliza anajisikiaje alisema ana
amani kabisa lakini niligundua haikuwa amani ya kristokwani amani ya kristo
huwa haina utata kwa ndani.. nilimpa ushauri wa kibiblia na kumpa wiki moja ya
maombi alipime jambo hilo mbele za Mungu. Nashukuru Mungu alimpa neema na
kumjulisha kuwa mahusiano aliyokuwa nayo si sahihi akaamua kuyavunja na baadaye
amani ya kristo ilijaa ndani yake. Mwaka jana mwezi wa pili alifunga ndoa
takatifu…” biblia inatofautisha amani ya kristo na ya dunia(Yoh 14:1…) hakuna
mahusiano ya mapenzi kati ya aliyeokoka na ambaye hajaokoka (2Kor 6:15-17).
Umemhakikisha
Mungu?
Hata kama mahusiano
yenu ni ya waliookoka wote ni lazima pia umhakikishe Mungu uone kuwa yeye ndiye
ameruhusu hayo mahusiano au la. Mpendwa jitahidi kumhakikisha mungu
katika maisha yako. Ni vyema kutambua kuwa si kila
aliyeokoka anaweza kuwa mke/ mme wako. Biblia inasema kuwa Mungu akatwaa ubavu
mmoja kutoka kwa Adam akamtengeneza Hawa mke wake (Mwa 1:26-27). Hivyo, kuna
mtu special wa kwako ambaye Mungu
amemwandaa kwa ajili yako. Mhakikishe Mungu kwa maombi na ishara, yaweza kuwa
isiwe mara moja(angalia alicho kifanya Gideoni( Amu 6:36)). Ukisha gundua kuwa
siyo Mungu mwombe Mungu akupe hekima ya kuyakomesha mahusiano hayo katika njia
ambayo haitaleta madhara yoyote kwako na kwa mwenzako.
NB: Ni hatari kubwa
kuendelea katika mahusiano ambayo unajua kabisa Mungu hajayaruhusu, eti, kwa
sababu unafikiria itakuwaje ukiyavunja, au mwenzako atakuelewaje? Kumbuka ndugu
yangu haya ni maisha yako hivyo usiyachezee baadaye ukaja kujuta, kwani Mungu
kama hajakubali hautakuwa na haki ya kumdai chochote baadae mambo yakiharibika
kwani ulijua unacho kifanya. Usifanye huruma isiyo sahihi leo ikakugharim
maisha yako yote. Ukumbuke pia kuwa hata makanisan kuna ma agent wa adui
wanaoletwa kwa lengo tu la kuwaangusha watumishi waliosimama katika Mungu hasa
kupitia MAHUSIANO. Hivyo ni vyema uwe makini katika kila hatua unayopitia.
Pia, kuvunja
mahusiano kuna gharama yake. Hii nitaizungumzia zaidi katika sehemu inayo fuata
ya somo hili inayosema ‘utafanya nini mahusiano yakivunjika?’
Je ni hitaji lako kwa wakati huo?
Ni lazima ujue kwa
kuchunguza kwa umakini kuwa ni hitaji lako kwa wakati huu kuwa na mke/mme. Je,
uko tayari kutoka moyoni na si kwa ushawishi wa watu? Je, si kwa sababu
umewaona rafiki zako wanaoa na kuolewa na wewe ukatamani? Ni muhim pia kujua
kuwa hilo lililo katika wakati wako lazima liendane na wakati wa Mungu (Yoh
11:1…..) usifanye jambo wakati usio wake kwani kila jambo lina wakati wake( Mhu
3:1…)
K u m b u k a…….
Hakuna haja ya
kulazimisha kupendwa kwani kama limepata kibali mbele za Mungu kupendwa
kutakuja automatically tu. Kumbuka pia hapa nazungumzia upendo na si tama kama
wengi wanavyo yachanganya mambo haya mawili.
Ndugu zangu, kwa
leo naomba niishie hapa, kesho ntakuletea mwendelezo wa somo hili katika vitu
hivi ‘utafanya
nini mahusiano yakivunjika?’ na ‘jinsi ya kuutambua upendo wa kweli’
Mungu wangu ninaye
mtumikia na Awabariki sanaa…
MZAWA WA INJILI
Kwa maombi na
ushauri tumia,
sekomu casfeta
tayomi blogspot.com
0759210407
No comments:
Post a Comment