1.0
UTANGULIZI
Tunamshukuru MUNGU aliyetuwezesha kwa
kipindi chote tulichokuwa katika uongozi tangu tulipochaguliwa tarehe
02.02.2013 hadi leo tarehe 01.02.2014.Ni ukweli usiofichika kwa nguvu zetu na
akili zetu tusingeweza kufanikisha yale tuliyopanga kufanya ila kwa msaada wa
MUNGU tumeweza kufanya. ( Zekaria 4:7).Shukrani zetu pia ziende kwa mchungaji
wetu mlezi, Mchungaji Chambo kwa kutulea vema kiroho na hata kimwil na
ametusadia sana kipindi chote cha uongozi wetu,bila kumsahau Mwalimu wetu mlezi
Madam Asnaty amekuwa msaada kwetu kipindi chote cha uongozi wetu.Tunawashukuru
viongozi wetu wa CASFETA,wilaya na mkoa,waratibu wa wilaya,mkoa Kanda na Taifa
kwa ujumla kwa kuwa wamekuwa sehemu ya
Mafanikio ya CASFETA.
2.0 UONGOZI
Viongozi
tuliokuwa madarakani katika kipindi cha mwaka 2013-2014 ni kama ifuatavyo.
·
FLAVIAN MASSAGO-Mwenyeki-------..
·
MINAELY KIKA-Makamu mwenyekiti
·
KAIZER MSOSA-Katibu…………… .
·
MELABI MPONGO-Katibu msaidizi
·
JOYCE RUKANDA –Mhasibu………………
·
JEREMIAH WILFERD –Mwenyekiti wa
maombi……….
·
ASHERY NICHOLAUS-M/M Maombi
·
MAX MEDARD-Mwenyekiti wa Uinjilisti…………
·
JULIETY PAUL-M/M Uinjilisti
·
FESTO SHIJA-Kiongozi wa kwaya
·
RESTITUTA SHABO-Kiongozi wa Elimu
·
JOYCE WILSON-Mwenyekiti wa wadada
·
SEBUYE ZAKAYO -Mwenyekiti wa wakaka
3.0
IDADI YA WANACASFETA
Tulikikabidhiwa
uongozi kukiwa na idadi ya wanachama 57.mwaka watatu wakiwa 26,mwaka wa pili 20
na mwaka wa kwanza 11.Leo hii tunakabidhi uongozi kukiwa na wanachama 63,mwaka
wa tatu wa sasa 23,mwaka wa pili wa sasa 12,mwaka wa kwanza wa sasa 26 na
masters wawili (2)
4.0
MALENGO
Kama uongozi
tulijiwekea malengo mbalimbali tukigawa malengo yetu katika makundi
mawili;malengo ya jumla na malengo ya Kila Idara
4.1
Malengo ya Jumla
Malengo haya yanatokana
na malengo ya jumla ya CASFETA TAYOMI
ü Kuwaunganisha
wanafunzi wote wenye imani za kipentekoste
ü Kuwafundisha
wanfunzi maadili ya kikristo
ü Kuwahimiza
vijana umuhimu wa kusoma kwa bidii
ü Kuwahamasisha
vijana juu ya agizo kuu la kumtumikia MUNGU.
4.2
Malengo ya Idara
Malengo haya yanatokana
na malengo ya idara zilizopo katika katika tawi letu
4.2.1
Idara ya Fedha
ü Kuhakikisha tunalipa madeni yote tuliyokuwa tunadaiwa.
ü Kuhakisha
tunalipa michango yote yote ya kitaifa kwa wakati sahihi k.m ada,AGM.JNLC
ü Tunaimarisha
mfuko wetu wa CASFETA
4.2.2
Idara ya Umbaji
ü Ununuzi
wa speaker kwa ajili ya sound kwa ujumla.
ü Kurekodi
album ya kwanza (audio) ya New Jerusalem choir
ü Kununua
wireless mic
ü Ununuzi
wa bass guitor
ü Ununuzi
wa sare za kwaya
ü Ununuzi
wa generator
ü Kuanzisha
idara ndogo ya fedha ,maombi na nidhamu ndani ya kwaya
ü Kufanya
mikesha ya mazoezi ya uimbaji
ü Kuboresha
huduma ya kusifu na kuabudu
4.2.3
Idara ya Elimu
ü Kufanikisha
elimu ya science na teknolojia kwa wana CASFETA inatumika vema katika maadili
ya KIMUNGU
ü Ufundishaji
wa masomo mbalimbali k.m education motivation
ü Kuhimizana
kuhusu kusoma kwa bidii
4.2.4
Idara ya maombi
ü Kutumia
siku ya ijumaa ya maombi kwa maombi ya mkesha
ü Kuendesha
midahalo ya wazikuhusu maombi na mambo mengine ya kiroho ili kupanua uelewa
zaidi.
ü Kuwa
na maaombi ya viongozi
ü Kuwepo
na maombi ya kufunga na kuomba angalau mara moja kwa mwezi.
4.2.5
Idara ya uinjilisti
ü Kuendesha
mikutano mbali mbali ya injili
ü Kuendeleza
vipindi vya mijadala juu ya mada mbalimbali
ü Kutembelea
wagonjwa na wafungwa
ü Kushuhudia
neno la
Mungu nje na ndani ya maeneo ya chuo
ü Outreach
4.2.6
Idara ya wakaka na wadada
ü Kuandaa
semina na workshop
ü Kusimamia
nidhamu kwa wakaka na wadada
5.0
MAFANKIO
Mafanikio pia
yamegawannyika katika makundi mawili,mafanikio ya jumla na kupitia idara
5.1
Mafankio ya jumla
ü Kuchangia
na kushiriki kongamano la Pasaka
ü Kuhudhuria
kikao cha vingozi kitaifa (JNLC) Dodoma mwez
June mwaka jana
ü Kuhudhuria
makongamano ya kiwilaya
ü Kuwaunganisha
vijana wa madhehebu mbalimbali ya kipentekoste
ü Kuhubiri
injili katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Lushoto
5.2
Mafankio ya idara
Mafanikio haya
yanatokana na malengo ya idara.
5.2.1
Idara ya Fedha
ü Kuimarisha
mfuko wa CASFETA
ü Kulipa
ada ya uanachama kwa wakati
ü Kuchangia AGM na JNLC
ü Kufanikisha
mahafali ya mwaka wa tatu mwaka jana ambapo meni rasmi akikuwa mkurugenzi mkuu
wa CASFETA taifa.
ü Kulipa
madeni yote tuliyokuwa tunadaiwa
ü Kuchangia
sherehe,na shughuli nyingine katika kanisa letu la hapa Magamba.
5.2.2
Idara ya Uimbaji
ü Ununuzi
wa speaker; Tumefanikiwa kununua speaker
2 mid kutokana na michango ya wanacasfeta
ü kurekodi
album; Mwishoni mwa mwaka 2013 tulifanikiwa kurekodi album ya kwanza audio
(nyimbo 8) ambayo iko tayari tumeshaisikiliza kwa mara ya kwanza ikiwa bado
inaendelea kufanyiwa tathmini zaidi zakiufundi ili iwe vizuri zaidi kihuduma.
ü kununua
Microphone;Mpaka sasa tayari tunazo wireless mic 2 tunamshukuru Mungu kwa hatua
hii
ü Idara
ndani ya Kwaya; Tayari tunazo idara 3 zilizo kamili zinazofanya kazi ambazo ni
fedha, maombi na Nidhamu
ü Huduma
ya Kusifu na kuabudu; tunnamshukuru Mungu huduma hii imeendelea kukua kwa
kufanya maombi ya pamoja ( yakufunga) , mazoezi kabla ya huduma, kuhudumu nje ya eneo letu, kuhimiza kusifu
katika roho na kweli na kubuni mbinu sahihi mbalimbali kwa ajili ya kumwinua
Mungu katika ibada zetu.
ü Mikesha
ya mazoezi; Juu ya hili tumefanya kwa sehemu kwa kile kipindi cha kuelekea
kurekodi ingawa sio katika ufanisi tulioulenga.
ü Unaweza
kuangalia video za nyimbo zetu katika YOU TUBE- click CASFETA SEKOMU
5.2.3
Idara ya Elimu
ü Masomo
ya ya education motivation yalifundishwa
5.2.4
Idara ya Maombi
ü Kuitumia
siku ya ijumaa kwa ibada ya mkesha wa maombi na kujifunza NENO la MUNGU
ü Kuwa
na maombi ya kufunga na kuomba kwa kila mwezi mara moja.
ü Maombi
ya viongozi kwa kila siku ya alhamisi
5.2.5
Idara ya Uinjilisti
ü Kutembelea
makanisa mbalimbali ya kipentekoste ambayo ni; Mkuzi.Mkuzi(bonde la Baraka),
Malindi, PAG Kwemakame na TAG Lushoto mjini.
ü Kujifunza
neno kwa njia ya mijadala,
ü Kufanya
mkutano wa injili,ambao ulifanyika Kwemakame(viwanja vya CCM) kuanzia tarehe
2/8/2013 mpaka tarehe 6/8/2013.
ü Kuwa
na mfuko wa kamati ya uinjilisti,ambao mpaka sasa una shilingi za kitanzania
49,800. Kabla yetu idara hii haikuwa na mfuko wenye kiasi chochote cha pesa.
ü Kwa
sasa unaweza ukasoma masomo mbalimbali katika blog yetu SEKOMU CASFETA, picha
na matukio mbalimbali ,au mahubiri
katika YOU TUBE
5.2.6
Idara ya wakaka na wadada
ü Kuwa
na semina kwa wakaka na wadada.
6.0
CHANGAMOTO
Changamoto
zimegawanyika katika makundi mawili, za jumla na changamoto katika idara.
6.1 Chagamoto Kwa
ujumla
ü Kujitoa
(commitment) kwa baadhi ya wanachama ni tatizo tofauti na idadiya wanachama
waliopo .
6.2
Changamoto katika idara
6.2.1
Idara ya Fedha
ü Bado
mfuko wetu haujawa na fedha za kutosha
kukamilisha malengo ya tawi.
ü Bado
wanachama hawajawa waaminifu katika michango
ya uanachama na ile ya kitaifa.
6.2.3
Idara ya uimbaji
ü Fedha
imekuwa changamoto sana kwetu kupelekea baadhi ya malengo yanayogusa kwa sehemu
kubwa fedha, kutofanikiwa kwa muda muafaka mfano ununuzi wa guitor, generator,
na sare
6.2.4
Idara ya Elimu
ü Tatizo
la ulipaji wa ada kwa baadhi ya wana CASFETA ,na bado hatuna mfuko wa Elimu.
ü Ufinyu
wa muda wa kujifunza mambo mbalimbali katika idara ya Elimu
6.2.5
Idara ya Uinjilisti
ü Ufinyu
wa muda. Baadhi ya malengo hayakuweza kukamilshwa kulingana na ufinyu wa muda
wa kuyatimiza malengo hayo. Mara nyingi
muda umekuwa mdogo sana na huo huo kuingiiana na ratiba za kawaida za ibada
hivyo kukosa muda maalum kwa ajii ya idara.
ü Kutunza
muda. Hii imekuwa ni changamoto nyingine hasa wakati wa outreach. Wana CASFETA wengi
wamekuwa wakishindwa kutunza muda, wamejikuta wakichelewa na kuwapa hali ngumu
viongozi wa uinjilistu hasa kufika kwa wakati katika ibada na kukabiliana na
madreva wa magari
6.2.6
Idara ya wakaka na wadada
ü Maadili
kwa baadhi ya wana CASFETA limekua taitizo na hivyo kukosa ushuhuda mzuri
ü Ufinyu
wa muda kukamilisha mipango ya idara
7.0
MAPENDEKEZO
7.1
Mapendekezo ya jumla
ü Kuzidi
kusimamia maono ya CASFETA TAYOMI
ü Kujitoa
kwa muda wetu,mali zetu,na akili zetu ili kutimiza malengo ya CASFETA
ü Maendeleo
ya CASFETA yanaanzwa kupimwa kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja kiroho
7.2
Mapendekezo ya Idara
7.2.1
Idara ya Fedha
ü Viongozi
wajao wazingatie malengo ambayo hayajafanikiwa
ü Viongozi
wafuatilie michango na wanachama wawajibke kutoa kwa wakati
7.2.2
Idara ya Uimbaji
ü Tunashauri
uongozi ujao waanze na yale yaliyochangamoto wakati wakipindi chetu kwa
mafanikio mazuri zaidi ya huduma hii
ü Kujitoa
kwa hali na mali pia ni siri ya mafanikio ya huduma hii
7.2.3
Idara ya Elimu
ü Kuanzishwa
mfuko wa iadra ya elimu ili kuwasaidid wenzetu wanaposhindwa kukamililisha
gharama za masomo.
ü Kuhimizana
umuhimu wa kusona kwa bidii na kutumia nafasi zilizopo kuendelea na elimu ya
juu zaidi k.m Masters na Phd
7.2.4
Idara ya uinjilisti
ü Kuweka
utaratibu maalum utakao wafanya watu wote wafike kwa wakati kipindi cha
outreach.
ü Kutafuta
muda maalum nje ya muda wa kawaida ili kukamilisha baadhi ya mikakati ya idara
ambayo haiwezi kukamilishwa kwa kufuata utaratibu wa muda wa kawaida kwa kuwa
ni mfinyu.
ü Kuhakikisha
mfuko wa uinjilisti unakaa na fedha wakati wote na fedha hiyo itumike kwa
makusudi yanayo eleweka katika idara na mbele za Mungu
7.2.5
Idara ya wakaka na wadada
ü Kuzidi
kuishi maisha ya ushuhuda kama mabalozi wa YESU.
8.0
HITIMISHO.
MUNGU akiwa upande wetu
ni nani aliye juu yetu? Tunamshukuru
MUNGU aliyetuwezesh kufanya hayo yote,na ambayo hatujakamilisha tunaamini
viongozi wajao watakamilisha kwa kuwa hayakuwa mawazo yetu ila ni ya MUNGU
mwenyewe.Mwanafalsafa mmoja akasema kuwa
“sometimes we agree to disagree” akimaanisha wakati mwingine tulikubaliana
hata yale ambayo kwa interest za mtu mmoja mmoja hazikubaliki.Tuzidi
kusimamia maono ya CASFETA TAYOMI,”Chage the life of the youth to change the
world”. GOD BLESS YOU ALL,…” Msigombane njiani, its near by Msoga”
N.B .Ripoti hii na ripoti
za akila idara kwa undani zaidi,zitapatikana kwenye blog yetu,Link www.sekomucasfeta.blogspot.com,type
sekomu casfeta kwenye google
Imeandaliwa na viongozi
wa CASFETA SEKOMU
…………………………………….. ……………………………
FLAVIAN MASSAGO KAIZER
MSOSA
MWENYEKITI-CASFETA KATIBU-CASFETA
No comments:
Post a Comment