Monday, June 2, 2014

SURA YA MUNGU- SEHEMU YA PILI





katika sura tofauti
………wiki iliyopita tuliona dhana ya sura ya MUNGU inavyoweza kutoeleweka miongoni mwa watu wengi hasa wasiomjua MUNGU katika uhalisia wake,na ndio maana ukimkuta mtu ukamwambia kuwa wewe ni mtoto wa MUNGU atakushangaa na hata anaweza  kukuuliza kuwa , YESU alikuwa, mwarabu mara mzungu iweje asifanane na wewe.Hayo ni baadhi ya maswali ambayo watu wengi wasiomjua MUNGU huyauliza.Katika mtazamo wa  kwanza tuliona  “UTAKATIFU” unavyotupa nafasi ya kufanyika watoto wa MUNGU,kwani unatuunganisha na huyo MUNGU ambaye ni Baba yetu.Wiki hii tutaangalia mtazamo wa pili unaohusu “SURA YA MUNGU”.
KIBALI
Maana rahisi ya neon hili ni ‘hali ya kukubalika au kuruhusiwa kufanya, kumiliki, kuwa na kitu flani’.Neno hili katika maana ya kiingereza inaweza ikatamkwa (acceptance, approval; permit, permission).Ikiwa unakubaliana na mtazamo huu wa kuwa hata sura za wanadamu zinatupa kibali katika mazingira tofauti itakuwa rahisi kuelewa kitu ambacho niatkielezea hapo chini.”.Binafsi nimewahi kuaminiwa na kupewa Fedha nyingi na watu ambao hawajawahi niona ila kwa kuwa waliponiona waliona sura yangu  imefanana na baba yangu” hapa kuna kitu cha kujifunza,sura yangu ililipa kibali cha kupewa fedha,lakini kama isingefanana na baba ingenipasa kutoa maelezo ya kutosha juu ya uhusiaono wangu na baba.Katika  Yohana 14:1-11,kuna majadiliaano hapo kati ya YESU na wanafunzi wake hasa Tomaso ambaye ametajwa hapo.YESU anajitambulisha kama “njia ya kumuona Baba”,hapo unajifunza nini? SURA YA MUNGU,inampa kibali cha kufanyika njia “daraja” la kumuona MUNGU.Na tumtazame Yusufu sasa katika Mwanzo 41:38 ambapo mfalme Farao anasema “tupate wapi mtu kama huyu? Mwenye  Roho ya Mungu  ndani yake”.Hapa kitu kilicho ndani ya Yusufu (SURA YA MUNGU) inampa kibali cha kukubalika hata katika nchi ya ugenini na kuaminiwa kupewa kazi ya uwaziri mkuu mtu ambaye alikuwa kijakazi na baadaye mfungwa.Habari ya tatu inamuhusu Esta,biti wa kiyahudi katika nchi ya ugenini (Esta 1,2:1-17) ni habari inayoelezea jinsi maisha ya Esta yalivyokuwa kabla ya kuwa malkia na hata namna alivyopata umalkia.Mistari ya kukumbuka # 15,17# mistari hiyo katika sura ya 2 inaonyesha jinsi Esta alivyopata kibali kati ya wanawake wote na tena machoni pa mfalme…..
Kwa maelezo hayo na mifano mingi mingi katika biblia  tena Roho mtakatifu akikuongoza kuelewa unaweza kuona ni jinsi gani ambavyo SURA YA MUNGU inatupa kibali.Ni ombi langu na liwe hivyo kwako tuwe na SURA YA MUNGU,kitu ambacho kitatupa kibali machoni pa MUNGU na wanadamu.MUNGU akamuuliza Kaini “ukitenda mema hutapata kibali?” (Mwanzo 4:7), tenda mema na utapata kibali.
Itaendeleaaa.

#kaizer xavier msosa# 0716047700.0759302486

No comments:

Post a Comment