JINSI YA KUWATAMBUA MANABII WA UONGO.....2
wapendwa wangu nawasalimu katika jina la Bwana Yesu. ninamshukuru Mungu tena kwa kuwa yeye ni mwema na ametupa tena nafasi baada ya muda mrefu tuendelee na somo letu hili jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo. katika sehemu iliyopita tuliona asili na chanzo cha manabii wa uongo. napenda niwaambie wapendwa kuwa , dunia iko mwisho kabisa kama wewe ni mtumishi wa Mungu kaa katika msimamo wa Mungu na usiyumbishwe na kila aina ya imani inayozuka kila iitwapo leo.
ni kawaida leo kumsikia mtu akijiita mtumishi wa Mungu huku akiupinga uweza wa Yesu na kujifanya kuwa na mafunuo mengine. mtu wa jinsi hiyo bila mjadala nasema hakutoka kwa Mungu. biblia inasema yesu ndiye njia, kweli na uzima na hakuna mtu anaweza kumuona Mungu kama hakupita kwa Yesu.( yoh 14:6)
muonekano na tabia za manabii wa uongo
manabii wa uongo kirahisi waweza kutambulika kwa muonekano na tabia kama zifuatazo
kwa nje huonekana ni watumishi wema na wenye haki (Math 23:28, Mak 7:15)
hupenda kujisifu na kutangaza viwango vya juu sana kiroho
hupenda kujionyesha kuwa watumishi maarufu sana wa kiroho waliopakwa mafuta na Mungu
wanapenda kuonekana kuwa ni watu na mafankio makubwa na kufuatwa na watu wengi (Mt 7:l21-23, Mt 24: 11, 24 , 2Kor11:13-15)
wanafanana sana na mafarisayo wa kale kwa kuwa;
ni wanafiki(Mt 23:25 )
ndani wamejaa maasi (Mt 23:28)
tabia za imani potofu
zinajifanya kukubali mamlaka ya biblia lakini huitafsiri vibaya
huthamini sana unabii na mafundisho ya viongozi wao waanzilishi kuliko biblia
hukazia sana kufundisha uponyaji wa mwili kuliko roho na baraka za mwilini kuliko za rohoni
daima huchanganya mafundisho ya kikristo na taratibu zingine za kibinadamu zikiwemo zile za mila na desturi
hufundisha mafundisho yao potofu na hupenda kuweka nyongeza katika neno la Mungu hata yako kinyume na biblia na hulazimisha watu kuamini tu kwa kuwa ni ufunuo
hufanya miujiza mingi kwa kutumia wengine kwa kutaja jina la Yesu huku wakitumia mbinu za viini macho
wengi hupuuza agizo kuu la Bwana Yesu la kuuendea ulimwengu kwa injili bali hupenda kuwaendea watu waliookoka tayari na kutaka kuwaongezea mambo kama masharti kwa ajili ya kupata wokovu
Mungu wa mbinguni na awabariki sana .... tutaendelea siku nyingine
ev maxwell medard (mzawa wa injili) 0759210407,,, medardmaxwell@yahoo.co.uk au medardmaxwell@gmail.com
No comments:
Post a Comment