"nabadilisha mwelekeo" |
Kwa wapenzi wa mpira najua,wanafamu mifumo mbalimbali ambayo hutumiwa na makocha ili kuhakikisha timu zao zinaibuka na ushindi mzuri.Katika hatua hii makocha huwa makini kuifahamu timu pinzani,akishaifahamu anapanga mfumo wa uchezaji utakao weza kuwadhibiti wapinzani wake.Ndio maana 1Wafalme 17,Mungu alipojua safari inyomkabili Eliya mbele yake alimwambi ainuke ale,hivyo alitambua ugumu wa "mchezo" ule ivyo aliweka mfumo mzuri utakaomfanya Eliya awe mshindi.
Kuna wakati yale tunayoyapanga hayaendi na tunabaki tusijue tuanzie wapi tena na tuelekee wapi tena,ndio maana akasema "Mambo mengine hayawezekani ila kwa kufunga na kuomba",hapo ikimaanisha kuwa kuna wakati ambao inakupasa ubadilishe mfumo uliouzoea kutumia na utumie mfumo ambao utakupa matokeo chanya.
ITAENDELEA
No comments:
Post a Comment