Bwana YESU asifiwe!!!!!!!
Ni kauli mbiu iliyobuniwa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikibeba matumaini ya matokeo makubwa katika sekta mbalimbali......Tumeipenda kauli mbiu hiyo nayo itatuongoza katika mwaka wa masomo wa 2013/2014.Tunahitaji matokeo makubwa kiroho kwetu binafsi tuweze kuongezeka kimo,upana wa kumjua yeye aliyetuita.Pia tunahitaji matokeo makubwa katika kuifanya kazi ya MUNGU zaidi tukiweza kuifikia jamii isiyofikiwa na NENO LA MUNGU ili kuitimiza vision ya CASFETA "CHANGE THE LIFE OF YOUTH TO CHANGE THE WORLD"...Matokeo makubwa hayo tunayatarajia katika masomo yetu pia tupandishe viwango vyetu...
Katika kuhakikisha matokeo makubwa yanapatikana sasa kama (Wafilipi 4 :6) inavyosema msijisumbue kaw Neno lolote bali katika kila jambo kusali na kuomba,ndivyo tulivyojipanga kwa kuanza na maombi Ijumaa hii na kila ijumaa ila tufikie lengo letu.Kuna msemo usemao "usianzishe safari na mtu asiyetaka kwenda atakuchelewesha njiani" hivyo tunapenda mpango huu utembee na watu walio tayari kwenda
KWA PAMOJA NA KWA UMOJA "We build the city of God"
No comments:
Post a Comment