Monday, May 27, 2013

KUMTOLEA MUNGU

Ndugu wapendwa nawasalimu wote katika jina la Bwana Yesu. tunayo furaha kubwa tena kuwepo kwa ajili ya kuendelea kuyatangaza maneno yaliyojaa tumaini na baraka ya bwana wetu yesu kristo. kabla sijakuletea somo la JINSI YA KUWATAMBUA MANABII WA UONGO litakalokuijia siku si nyingi kadri bwana wetu Yesu anavyotupa kibali, leo ningependa kushirikiana na wewe maneno machache yatakayokutia moyo na kukupa nguvu ya kuendelea mbele zaidi katika kumtumikia Mungu. kwanza kabisa niseme kwamba blog yetu hii ni blog ya ufalme wa Mungu hivyo tegemea mafunuo mapya kutoka kwa M UNGU kupitia blog hii. leo hii ningependa kuzungumzia na kukukumbusha mpendwa msomaji wetu kuhusu umuhimu wa kumtumikia Mungu kupitia matoleo yako. kumekuwa na minon'gono mingi kuhusu utoaji. wengine wameona wachungaji wakizungumzia habari ya matoleo ni kama wanataka pesa tu na si agizo la Mungu. lakini ukweli ni huu mpendwa, kumtolea Mungu ni agizo la Mungu na si kama inavyotafsiriwa na watu wengi hivi sasa. ili mtu abarikiwe ni lazima amtumikie Mungu kwa matoleo mengi. kuna ushahidi mwingi katika biblia kuhusu jambo hili. japo yapo mengi sana lakini nakukumbusha tu habari ya kaini na habili na ni nani kati ya hao alibarikiwa na ni nani hakubarikiwa kwa sababu  ya utoaji. licha ya kubarikiwa biblia pia inaagiza watu watoe kwa kuwa kila ilipo hazina yako ndipo na roho yako itakapokuwa. hivyo nakusihi ujisikie amani katika kumtolea Mungu na ujenge tabia ya kutoa kwa kiwango cha kuugusa moyo wa Mungu. Mungu akitujalia tutajifunza masomo ya kumtolea Mungu pia. Mungu akubariki. nawe msomaji wangu ambaye haujaokoka bado, ningependa utambue hatari ya kuishi bila kumfanya Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. nakusihi basi mpokee Yesu leo nawe utakuwa salama. hebu tamka maneno haya hapa chini kwa imani nawe utaokoka
     bwana yesu............
    niko mbele zako...........
   nimetambua makosa yangu........
   naomba unisamehe sasa............. uniandike katika kitabu cha uzima...........
                unipe nguvu ya kukufuata wewe siku zangu zote.........
                unipe na roho wako mtakatifu................
A             M           I               N                  A,,,, sasa umeokoka, usitende dhambi tena.....
                  katika shamba la Bwana
                           ev: maxwell
                                  mzawa wa injili

No comments:

Post a Comment