VIEW
POINT
v Ufahamu
Unaweza ukaeleza ufahamu kwa lugha na maana nyingi.Tafsiri
ya Oxford inaeleza ufahamu (understand) kama (perceive the intended meaning of words, a language, or a
speaker).Ufahamu unaletwa na maarifa (knowledge) na hayo maarifa ni NENO na
hilo NENO ni YESU mwenyewe.Hosea 4:6 anasema watu wangu wanaanamizwa kwa kukosa
maarifa ambayo ni NENO la MUNGU.Yohana 1:14 anasema “Neno alifanyika mwili
akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake……”akimaanisha YESU KRISTO.Kanisa
limekosa maarifa ya ki MUNGU ambayo ndiyo maongozo yake.Maarifa yakipotea ni
kama mifugo iliyokosa mchungaji kwani utawanyika bila mwelekeo maalumu
v Kusimama
katika mpango (Goal) wa MUNGU
Musa alilijua kusudi la MUNGU la kumwita (Mwanzo 3:10), hata
vikwazo (Mwanzo 14:15-16) vilipokuja juu ya kusudi la MUNGU kuwakomboa
Israeli,alisimama na kuamini MUNGU aliyemwita atakamilisha lile aliloahidi
kwake.
Yusufu naye alilljua kusudi la MUNGU,(Mwanzo 37:9).Ingawa
alipata vipingamizi vingi(Mwanzo 39:7-9),alizidi kusimama katika kumwona MUNGU
atomize ndoto ile aliyoiota.
Kanisa limeshindwa kujua kusudi la MUNGU,la kuwekwa mahali
lilipo ndio sababu maendeleo yake yamedumaa.
HITIMISHO
§ Lengo kubwa la kanisa ni kumzalia MUNGU
matunda (Marko 16:15).Kutokuwa na UFAHAMU kwa kanisa na kushindwa kujua kusudi
la MUNGU kwalo vimechangia kwa kiasi kikubwa sana kwa kasnisa kutofikia ule
utukufu ambao Nabii Hagai katika (Hagai 2:9) anasema utukufu wa mwisho utakuwa
mkuu.Kanisa linatakiwa liwe mji/sehemu ya makimbilio kwa watu mbalimbali na
wenye mahitaji mbalimbali.Tazam YESU alivyofuatwa na kusanyiko kuu (Marko
10:1)………………………..Wewe kama kanisa umefuatwa na watu wangapi toka mwaka huu uanze
wa 2013? Tafuta maarifa ya ki MUNGU upate ufahamu,pia tambua kusdi la MUNGU
kwako ili Ahadi ya MUNGU kwa kanisa itimie kwako.Rejea Mika 4:1-2, Ezekieli 17:22.
LORD HAVE YOUR WAY IN
YOU
Says Kaizer Xavier Msosa 0716047700,0759302486
No comments:
Post a Comment