kila mtu na sura yake |
.................Zamani
nilikuwa najiuliza maswali mengi,najua
hata wewe ulijiuliza au yamkini unajiuliza maswali hayo kila siku kuwa MUNGU
kafanana vipi na mwanadamu ikiwa Biblia inasema kuwa “………na tumfanye mtu kwa
mfano wetu na sura yetu ….” (Mwanzo 1:26).Hajaishia hapo tu katika injili ya
Yohana 1:12 Biblia inazidi kumuweka karibu mwanadamu na MUNGU kwani inaonyesha
jinsi mtu akimkubali MUNGU anafanyika kuwa mwana wa MUNGU….Kama hali ni hiyo
sura ya MUNGU kama baba itafanana na mchina, mzungu, mwafrika au mhindi? Yule
mheshimiwa aliyeigiza video ya maisha ya YESU amechukua umaarufu mkubwa duniani
na hata watu wengine wameamini kuwa YESU yupo vile, kama hali ipo ivo kuna
umuhimu wa kuijua sura ya MUNGU. Katika somo hili tutaenda kuangalia sura ya
MUNGU katika mtazamo wa kibiblia zaidi,kwa nini ameonyesha umuhimu wa sisi kuwa
na sura yake.Kuna mtu napendaga kumwambia “as mother as daughter, as father as
son” na hili linathibitishwa na maneno haya katika Injili ya Yohana 5:19 ampapo
biblia inaonyesha kuwa mwana hawezi kutenda jambo lolote mwenyewe isipokuwa
amemwona baba akitenda.Hapo imeonyesha uhusiano wa mwana (YESU) na baba (MUNGU
BABA)……
UTAKATIFU
Biblia
inaeleza wazi katika 1Petro:15-16
“iweni watakatifu kama mimi nlivyo mtakatifu” inamaanisha nini hapo? Ni
ishara kuwa MUNGU wetu ni mtakatifu na hata sura yake imejaa utakatifu.Mtazame
Manoa baba wa Samsoni katika kitabu cha Waamuzi 13:22,alivostuka na kupatwa na
mshangao alipomuona tu malaika wa BWANA sura yake tu ilimuweka mbali nay eye
hata akajiona kuwa atakufa.Mtazame Musa katika Kutoka 33:11 jinsi biblia
inavyonesha ukaribu wetu na MUNGU unajengwa kwa kuwa na sura ya MUNGU hivyo
ilimuwezesha Musa kuongea na MUNGU kama mtu na rafiki yake.Ukikosa utakatifu
basi umepoteza sura ya MUNGU ndio maana Adam na Eva walipomuasi MUNGU walijiona
wapo uchi wamekosa sura ile ya MUNGU hata wakaanza kujitafutia mavazi ya kuvaa
(mwanzo 3:7)……
Itaendelea!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kaizer
Xavier Msosa-0716047700,0759302486
No comments:
Post a Comment