Ndugu wapendwa shalom.... ninamshukuru Mngu kwamba leo tumepata kibali tena kw ajili ya kushirikishana maneno ya uzima. Katika siku ya leo imempendeza M UNGU tuweze kulianza somo letu la jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo.
utangulizi
unabii ni huduma kati ya huduma tano alizoziacha Bwana Yesu. Ni kweli kuwa huduma hii imepata vikwazo vikubwa katika utendaji wake naweza kusema hata zaidi ya huduma zingine. Neno manabii wa uongo limekuwa likilindima katika kila kona ya nchi hii. Wengine katika nyumba zao za ibaada wamekuwa wakifundisha na kusema kuwa ''hakuna nabii wa Mungu kwa sasa, manabii walikuwa enzi za agano la kale''. Hii ni kutokana tu na uelewa mdogo, ama hasira kutokana na matokeo mabaya waliyokumbana nayo kutokana na uwepo wa manabii wa uongo. Ukweli ni kwamba, manabii wa Mungu wapo na manabii wa uongo pia wapo , kilichopo, ni namna ya kuwatambua manabii hawa wa uongo na kujua namna ya kuwaepuka kama tutakavyoona katika somo hili.
manabii wa uongo hutoka wapi?
NI swali linalo sumbua vichwa vya watu wengi sana. manabii hawa wa uongo huanzia na hutoka wapi? manabii wa uongo wana asili zinazotokana na vyanzo vikuu vifuatavyo;
1. watu wa adui ingawa walikuwa kanisani lakini ukweli ni kwamba walipandwa humo na shetani kusudi waitimize kazi ya adui( mat 13: 24-28 , 36-43, mdo 20:29)
2. wapo walioanza vizuri kama watumishi wa Mungu. Kwa sababu hiyo walifaulu kujiaminisha kwa watu na baadaye wakaharibika kwa sababu mbali mbali kama vile tamaa ya pesa n.k (ef 5:5-6, 1yoh 2:18-19, mdo 20:30)
3. watu walioasi hivyo baadala ya kuutubia uovu wao waliendelea katika hali hiyo hiyo na kuendelea kujiita watumishi wa Mungu.kwa sababu hiyo, wanatafuta kila nguvu kiroho ili waendelee kuwateka watu kwa miujiza.
kwa leo naomba tuishie hapo na tukutane tena kipindi kingine katika mwendelezo wa somo hili...
ubarikiweeeeeeeee............
ev: maxwell
mzawa wa injili
0759210407 medardmaxwell@yahoo.co.uk, medardmaxwell@gmail.com
No comments:
Post a Comment