IDARA YA UINJILISTI SEKOMU CASFETA TAYOMI
IDARA YA UINJILISTI SEKOMU CASFETA TAYOMI
Tunayo furaha kubwa kuwakaribisha wapendwa wetu wasomaji na wadau wa blogi hii. tunapenda kuku hakikishia kuwa hautabaki kama ulivyo kuwa kama ukipata muda wa kuitembelea blog yetu walau kila siku. katika mwaka huu wa masomo 2012/2013, idara ya uinjilisti tunayo mipango na mikakati madhubuti katika kuhakikisha kuwa tunawaleta watu wengi kwa yesu kama lilivyo agizo kuu la bwana wetu yesu kristo (mk 16:15....). kwa hiyo kuihubiri injiri ni lazima kama kutimiza agizo na si hiari kama wengi wanavyo dhani. chini ya ev: MAXWELL M na ev:JULIETH P kwa uongozi mkuu wa Mungu baba, Mwana na Roho mtakatifu ,tunapenda kukushirikisha mipango yetu na mikakati yetu hadi ifikapo mwisho wa semester hii. baadhi ya mipango na mikakati yetu ni kama ifuatavyo.
kuhubiri injiri kupitia kuwashuhudia watu habari njema za bwana wetu yesu kristo. kazi hii itafanywa na wana casfeta wote katika maeneo yao husika wanayokaa yaani msheremle, coast, bondeni na mjini. tunatarajia msaada mkubwa wa Mungu katika eneo hili na tunategemea taarifa njema za matendo makuu ya bwana yesu kutoka kwa wana casfeta wote mara zitakapo hitajika.
kuwafanya watu wasome neno la Mungu kwa bidii kwa kutoa 'biblical assignment' na hivyo kuweza kumshinda adui shetani kwa neno.
kufanya mkutano wa injiri mara ifikapo mwisho wa semester hii. mkutano huu utaandaliwa na wana casfeta wote kwa kushirikiana na watumishi wa Mungu katika maeneo husika ya mkutano.
kuyafikia maeneo ambayo hayajafikiwa bado kwa ajiri ya kuyatangaza maneno ya Mungu
kuwatembelea wagonjwa, wenye shida na waliofungwa na nguvu za giza kwa lengo moja tu la kuwatoa katka utumwa wa dhambi na kuwaleta kwa yesu.
outreach programs ni kama kawaida katika kuhakikisha casfeta wanatumika kikamilifu kwa Mungu wao. outreach ni kwa wana casfeta wote.
hii ni baadhi tu ya mipango yetu kati ya mingine mingi tuliyonayo. pamoja na hayo , usikose kusoma na kujifunza masomo mengi yatakayo kujenga na kukuimarisha kiroho kupitia blogi hii.
kaa chonjo na somo la' jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo' litakalokuijia hivi karibuni.
katika shamba la Mungu ni mimi 'MZAWA WA INJILI'
ev: MAXWELL M
mungu awabariki.....................!
kwa maelezo na msaada zaidi wasiliana nasi, 0759210407 au 0763411845, email medardmaxwell@yahoo.co.uk au medardmaxwell@gmail.com
No comments:
Post a Comment