SEHEMU YA KWANZA (1)
Fikiria unaanza safari ya kuelekea mahali Fulani pasipo
kufahamu (eneo) tena huna mtu wa kukupokea!!!!!Uhakika wa safari yako unakuwa
ni mgumu.Si katika maisha ya kawaida tu bali hata katika maisha ya kiroho na katika huduma ambazo M UNGU ameweka ndani
yetu.Makubaliano ni msingi wa mafanikio ya safari ya mtu na mtu.Petro alipoanza
safari ya utumishi (uanafunzi) kwa ujasiri alimuuliza Yesu ‘tumeacha vyote
tumekufata wewe tutapata nini ?”Mathayo 19:27 .Hii ilionesha kuwa Petro
alitaka ayaone mapatano baina yake na
aliyemuita(YESU) katika safari ile.Yesu akamjibu Mathayo 19: 28 -29 kuonesha makubaliano baina yake na Petro.Je umeweka
makubaliano(mapatano) na nani katika safari unayoiendea?
Angalia Musa anaitwa kwenda kuwakomboa Israeli,Mwanzo
3:10.Musa anaanza kwa kuuliza maswali muhimu juu ya safari yake,Mwanzo
3:11.Hatua hii ya maongezi kati ya Musa na MUNGU inaonesha makubaliano (mapatano)baina
ya MUNGU na Musa.Katika lugha ya kiingereza tunaweza tukaita (terms and
condition) ambazo hufikiwa na watu wanaoingia mkataba ( contract).
AGANO NI NINI?
Jibu rahisi ni mapatano baina ya watu wawili au
zaidi ambayo kila upande utalazimika kufuata masharti (terms and condition)
waliyokubaliana.Upande mmoja ukishindawa kufanya yaliyo katika makubaliano
unastahili kulipa gharama au kudaiwa ufanye lililowapasa kufanya.
ITAENDELEA
Kaizer Msosa
No comments:
Post a Comment